Thursday, September 20, 2012

RUFAA YA LEMA YASOGEZWA MBELE MPAKA OKTOBA 2, 2012



Godbless Lema akiwasili viwanja vya Mahakama Kuu Arusha kusikiliza rufaa yake mapema leo asubuhi.
 
Sehemu ya umati wa wakazi wa Arusha waliofika eneo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa hiyo.
Shauri lililofunguliwa na aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaaa nchini kupinga kuenguliwa kwake kuwa mbunge limeahirishwa hadi tarehe 2 mwezi ujao litakaposikilizwa tena.
Mapema asubuhi ya leo mamia ya wafuasi wa Chadema walijitokeza katika eneo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa hiyo ambayo ilisikilizwa kwa muda mrefu kiasi kabla ya kuahirishwa.
Taarifa za awali kutoka mahakamani hapo kabla ya kusikilizwa kwa shauri hilo hii leo zilieleza kuwa tayari mawakili wa pande zote mbili walishaandika barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hilo hadi Oktoba 2, mwaka huu, kufuatia mawakili, Tundu Lissu, anayemtetea Lema na kaka yake, Alute Mughwai, anayewatetea walalamikaji, kufiwa na baba yao mzazi.
Imeelezwa kuwa, upande wa walalamikaji wameweka mapingamizi fulani ambayo jopo la majaji litayapitia hiyo tarehe 2 oktoba. Taarifa nyingine ambayo haijaweza kuthibitishwa na Blog hii zinaeleza kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa hukumu ya rufaa hii kusomwa Dar es Salaam...






BONGO NI NOMA........







Hoteli ya Singita Grumeti Reserves.

Stori: Mwandishi Wetu
HOTELI ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania.
Singita ndiyo hoteli nambari moja duniani, ikichukua tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na taasisi maarufu ya Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya utalii duniani.
Hoteli hiyo, inathibitisha kwamba thamani ya Tanzania ipo juu mno, ndiyo maana mwekezaji kutoka Afrika Kusini, Luke Bailes, aliamua kufanya uwekezaji wa hali ya juu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Matokeo hayo, yaliandikwa Agosti mwaka huu kwenye jarida maarufu kwa kuchapisha matukio ya biashara za utalii, linaloitwa T+L Magazine. Jarida hilo linamilikiwa na Taasisi ya US Travel + Leisure.
Tangu kufunguliwa kwake, Singita Grumeti imekuwa kivutio cha viongozi, matajiri na watu maarufu ambao mara kwa mara hutinga kujivinjari, vilevile kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Kwa mujibu wa US Travel + Leisure, sababu ya kuipa Singita hadhi ya kuwa hoteli namba moja duniani, inatokana na muundo wake, huduma zinazotolewa, kuwa ndani ya mbuga kubwa kabisa ya wanyama duniani (Serengeti), vilevile wageni mashuhuri inaopokea.
Inaelezwa kwamba Singita Grumeti ndiyo hoteli inayoongoza kwa sasa duniani kwa kupokea wageni wenye hadhi ya daraja la kwanza, wakiwemo marais, matajiri, wanamichezo, wasanii, viongozi mbalimbali maarufu ulimwenguni na kadhalika.

HAWA WANATAJWA KUJIVINJARI SINGITA
Marais wa 42 na 43 nchini Marekani, Bill Clinton na George W. Bush, kwa nyakati tofauti wamefikia kwenye hoteli hiyo baada ya kuvutiwa na sifa zake zinazotikisa duniani.
Bilionea wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich, alipotembelea nchini Septemba 2009, inaelezwa kwamba alilala kwenye hoteli hiyo.
Bilionea wa Kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa ni tajiri namba 19 duniani, alifika nchini mwaka jana na kufikia kwenye hoteli hiyo.
Wakati alipowasili nchini, Mekesh alikuwa tajiri namba nne duniani. Ripoti ya mwaka 2011, ilimtaja kuwa tajiri namba tisa na sasa anashika nafasi ya 19.
Mke wa zamani wa mwanasoka anayechezea Chelsea ya England, Ashley Cole, Cheryl, alipofika nchini miaka miwili iliyopita, inaelezwa pia kwamba alifikia kwenye hoteli hiyo.
Mwanamitindo aliye pia mcheza sinema maarufu wa Hollywood, Marekani, Angelina Jolie na mumewe Brad Pitt, waliripotiwa kufika nchini na moja kwa moja makazi yao yakawa Singita Grumeti.
Wengine ambao wanatajwa kuwahi kupumzika kwenye hoteli hiyo ni mwanamuziki wa Marekani, Sean Carter ‘Jay Z’, mwanasoka Thierry Henry, Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa orodha ya wageni wanaofikia Singita ni kubwa mno, tatizo hufanywa siri kwa sababu watu wengi mashuhuri ulimwenguni huwa hawapendi ijulikane kama wamefikia kwenye hoteli hiyo kwa sababu za kiusalama.



 

 

KUWA MAKINI BARABARANI EPUKA AJALI

AJALI nyingi za barabarani nchini husababishwa na madereva wazembe wasio zingatia sheria za matumizi sahihi ya barabara. Miongoni mwa ajali hizo nyingi husababishwa na madereva hao kuovatake magari mengine katika kona au milima kama basi hili linavyofanya katika kona ya Lugalo mkoani Iringa. Madereva “PAMBANA
NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.

Basihili lingine nalo lilikuwa linafanya makopsa hayohayo ya kulipita gari linguine katika miinuka na kona kali za mlima Kitonga.
Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Iringa, akiwepo RTO, SP. Pamphil Honono (kushoto) walimuona na kumsimamisha dereva wa basi hilo. Matukio haya yanatokea ndani ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa. 
 
Dereva huyo alikuwa ni Issack Gerald Nyamaiswe Mkazi wa Mjini Dodoma.  
 Nahapa Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani akimwandikia Notfication dereva huyo. 






P SQUARE HAO....



MANIZLE BWAI NA SUMALEE

No comments:

Post a Comment