Dodoma Kumekucha
Friday, August 30, 2013
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia amewataka watendaji wa wizara yake wanaoshiriki katika mitandao ya kubeba wabadhirifu ndani ya ofisi hiyo kujipima na kujiondoa wenyewe.
Na.Bilson Vedastus, Dodoma
Ghasia amebainisha hayo wakati wa hafla fupi katika kuwakaribisha watendaji wa wizara hiyo iliyofanyika mjini Dodoma.
Amesema hivi sasa ndani ya Tamisemi kuna mitandao ya kulea wabadhirifu na kumtaka kila mtu kujipima mahali alipo ili kuondoa kasoro hizo.
“Sasa nataka nisema kuwa kwa mtumishi au mtendaji ambaye hatakwenda na sisi tutahesabu kosa na hatutabembeleza mtu , tunataka kila mtu atimize wajibu wake katika eneo lake na hapa sitamwonea mtu na hatupo tayari kumbeba mtu.” alisema.
Alisema kwa muda mrefu amefanya kazi na timu ambayo ilikuwa haijakamilika jambo ambalo lilimfanya kufumbia macho baadhi ya mambo.
Alisema kukamilika kwa uteuzi wa Katibu Mkuu na manaibu makatibu wakuu wa wizara hiyo, kunaifanya timu kukamilika.
Lakini pia aliwataka makatibu wakuu hao waliopewa dhamana na Rais kusimamia sekta mbalimbali ndani ya wizara hiyo kuacha kujifungia maofisini na badala yake watoke na kwenda mikoani na wilayani kufuatilia kero za wananchi na kuzipatia ikiwa ni sambamba na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu mpya wa Tamisemi, Jummane Sagine, alikiri kuwapo kwa mitandano hiyo ya ubadhilifu ndani ya wizara hiyo.
“Kweli vitendo hivi vya mitandao na hata ubadhirifu niliviona kwa macho yangu na wakati mwingine niliambiwa lakini nilikuwa mpole katika kipindi hicho cha kukaimu,” alisema.
Aliwaonya baadhi ya watendaji wanaofanya ubadhirifu kwa ajili ya tamaa ya fedha kuacha.
Vilevile Katibu aliwaonya watendaji ndani ya wizara hiyo kuachana na porojo za siasa ndani ya ofisi hiyo ambayo ni muhimu kwa jamii.
"Si ajabu yaani kwa CCM tu, mbona nanyi chama chenu kilifanya hivyo ingawa mbunge wenu bado ni mbunge?,"
MZIMU wa kutimuliwa kwa aliyekuwa Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansour Yussuf Himid (CCM), umeibukia bungeni baada ya Mbunge wa Micheweni, Haji Khatib Kai (CUF), kudai kuwa kufukuzwa kwake ni kinyume cha Katiba ya nchi. Kai, aliseyasema hayo jana alipokuwa akiuliza swali kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambapo alisema Ibara ya 18 ya Katiba imetoa uhuru kwa mwananchi yeyote kujieleza ili mradi havunji sheria.
Kabla ya kujibu swali hilo, Pinda alimtaka mbunge huyo kutaja jina la kiongozi anayemzungumzi, ndipo mbunge huyo alipomtaja Mansour na kuwafanya wabunge kuangua kicheko.
Pinda alilijibu kwa kifupi huku akimrushia kijembe mbunge huyo kwa kusema kwamba si jambo la ajabu mwakilishi huyo kufukuzwa mbona chama cha CUF kilimtimua mbunge wao.
"Si ajabu yaani kwa CCM tu, mbona nanyi chama chenu kilifanya hivyo ingawa mbunge wenu bado ni mbunge?," alihoji Pinda kwa kifupi.
Agosti 26, mwaka huu Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) ilitangaza kuridhia kuvuliwa uanachama kwa Mansour kama ilivyopendekezwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Hatua hiyo, ilitokana na mjumbe huyo kukabiliwa na tuhuma akidaiwa kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama. Mengine kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka maadili ya CCM na Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015.
Agosti 18, mwaka huu Kamati ya maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, ilipitisha mapendekezo ya kumvua uanachama mwakilishi huyo na waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Thursday, August 29, 2013
SPIKA MAKINDA AINGIA KATIKA ORODHA YA WANAOTARAJIA KUWANIA URAIS
Na Bilson Vedastus - Dodoma
Harakati za kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimeanza kuchukua sura mpya, baada ya baadhi ya vigogo kujitokeza hadharani kumpigia debe Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Vigogo hao ambao wana ushawishi ndani ya CCM walishindwa kujizuia na kulazimika kumpigia debe Makinda ndani ya ukumbi wa Bunge jana, huku wakimwagia sifa za kuwa Rais wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kwa mujibu wa kikatiba.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Anna Abdallah, alimmwagia sifa spika huyo kuwa anafaa kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) na waziri kwenye serikali ya awamu ya pili na ya tatu , alitoa kauli hiyo alipokuwa akiunga mkono hoja ya Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Afrika (CPA) tawi la Tanzania Mussa Azzan Zungu, kumpongeza Spika Makinda kwa kuteuliwa kuwa Rais wa chama hicho Afrika.
Anna Abdallah, ambaye pia aliwahi kushika wadhifa wa ukuu wa mkoa katika utawala wa awamu ya kwanza, alisema uteuzi wa Spika Makinda, siyo heshima kwake tu bali ni kwa Watanzania wote, lakini hasa kwa wanawake.
Alisema haoni sababu ya kwa nini Spika Makinda sasa asigombee CPA ngazi ya kimataifa kwani yeye pamoja na Watanzania na wabunge kwa ujumla watamuunga mkono.
Alisema kwa msingi huo, anamshauri Spika Makinda kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha ndani na nje ya nchi kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kwa upande Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, wa Rungwe Mashariki, alisema Spika Makinda amekuwa mfano mzuri wa kuigwa kutokana na uongozi wake tangu akiwa mkuu wa mkoa, mbunge, naibu waziri, waziri kamili, naibu spika na sasa spika.
Profesa Mwandosya ambaye pia ni Mbunge wa Rungwe Mashariki akiwa amejitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka 2005 na kuishia kwenye nafasi ya tatu bora kabla ya yeye na Dk. Salim Ahmed Salim kubwagwa na Rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano mkuu wa CCM, alimwelezea Spika Makinda kuwa ni mtu mwadilifu, mtenda haki, anayejiamini, mvulimivu, mnyenyekevu, msikivu na mwenye msimamo, hivyo hashangai kupitia yeye (Spika), Bunge lijalo hata bila ya Katiba mpya, wanawake watafikia asilimia 55 katika Bunge.
Profesa Mwandosya alisema hiyo inatokana na ukweli wa historia yake ya uongozi wasichana wengi sasa wanataka kuwa viongozi, lakini pia wanawake wengi watajitokeza kugombea ubunge.
Hata hivyo, Profesa Mwandosya hakutaja moja kwa moja kama Spika Makinda anapaswa kugombea urais mwaka 2015, isipokuwa alisema kwa wale wanaofikiria 2015 watambue kwamba (Makinda) ni tishio kwao.
Kupigiwa debe kwa Makinda kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kunaongeza idadi ya makada wa CCM wanotajwa kuwania uteuzi wa chama hicho tawala.
Hadi sasa wanaotajwa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta; Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Wednesday, August 28, 2013
Watu milioni mbili nchini wakadiriwa kuwa wana ugonjwa wa kichocho
Na Elizabeth Joseph,Dodoma.
IMEELEZWA kuwa jumla ya watu Milioni Mbili wamebainika kuwa na ugonjwa wa Kichocho Nchini.
Hayo yalielezwa juzi na Daktari Kitengo cha Kichocho na Matende Dk.Phenehas Machumu katika Manispaa ya Dodoma wakati akitoa elimu juu ya ugonjwa huo katika kikao cha Wazazi kilichofanyika katika Shule ya Msingi Amani iliyoko Manispaa ya Dodoma Mjini kilicholenga kujadili Utoaji wa dawa za ugonjwa huo kwa watoto walioko shule.
Machumu alisema kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanasayansi imebainika kuwa idadi ya watu waliokutwa na tatizo hilo ni Milioni Mbili Nchini ambapo kwa Dunia nzima ni Milioni tano na kuongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kutokomeza ugonjwa huo.
Aidha aliwataka wananchi kuwa wepesi wa kupima afya zao katika magonjwa yote ili kujua kama wana maambukizi ya ugonjwa huo kwakuwa unaweza kuonekana kwa muda wa miaka kadhaa hali inayosababisha wengine kupoteza maisha bilakujua kama wana tatizo hilo.
Machumu pia alibainisha kuwa kwa Mkoa wa Dodoma mzunguko wa ugonjwa huo umefika asilimia 30 jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa wakazi wake hivyo kuwaomba wananchi kuungana na Wizara ya Afya katika kutoa elimu juu kutokomeza tatizo hilo na hatimaye kupunguza asilimia hiyo.
Pia aliwataka wazazi kujiandaa kisaikolojia kwa kukubali watoto wao kupewa dawa ya ugonjwa huo ili kutibu na kukinga maambukizi ya tatizo hilo kwakuwa katika kikao hicho wazazi wengi walionekana kuingiwa na hofu juu ya dawa hizo kwa kuhofia madhara yanayoweza kujitokeza mara baada ya mtoto kupewa dawa hizo kwakuwa mwaka 2011 wakati wa utoaji dawa hizo baadhi ya wanafunzi katika shule kadhaa walianguka kwa kizunguzungu,kichefuchefu na usingizi.
Kampeni dhidi ya Kichocho Kitaifa ilianza mwaka 2011 kwa kuwapa dawa za kinga watoto walioko Shule za Msingi wenye umri wa miaka mitano hadi kumi na nne kwakuwa imebainika kuwa wao ndio wako katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo kutokana na mazingira wanayokutana nayo ambapo kwa Manispaa ya Dodoma zoezi la ugawaji wa dawa hizo litafanywa Agosti 30 Mwaka huu katika Shule zote za Msingi.
CHELSEA INATARAJIA KUMPOKEA ETO’O NDANI YA MASAA 48... HUKU MOURINHO AKIMKUBALI KULIKO WOTE TORRES BA NA LUKAKU
Chelsea
iko kwenye hatua za kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o
kutoka Anzhi Makhachkala na dili hilo linatarajiwa kukamilika ndani ya masaa
48.
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Cameroon utakuwa mfupi wa kipindi cha mwaka mmoja.
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Cameroon utakuwa mfupi wa kipindi cha mwaka mmoja.
Eto'o alianzia soka yake Ulaya katika
klabu ya Real Madrid, lakini alicheza mechi tatu tu na akapelekwa kwa
mkopo katika miaka yake minne na klabu hiyo ya Jiji la Hispania.
Alitengeneza jina alipokuwa akichezea
Mallorca kabla ya kusajiliwa na Barcelona. Aliiwezesha kushinda Ligi ya
Mabingwa, akifunga dhidi ya Arsenal katika Fainali mwaka 2006.
Baadaye akaenda kuungana na Jose
Mourinho Inter Milan, na hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchaua kutua
Chelsea. Kocha huyo Mreno anaweza kuwa na imani naye zaidi kuliko
washambuliaji wake wa sasa, Fernando Torres, Romelu Lukaku au Demba Ba.
Tuesday, August 27, 2013
Wayne Rooney atakiwa ndani ya saa 48 baada ya kung'ara jana usiku
BAADA ya kunusurika kichapo katika himaya ya Mabingwa wa England Manchester United Jana Usiku baada ya Chelsea kupata Sare ya 0-0 Uwanjani Old Trafford Wayne Rooney akiwa nyota, Jose Mourinho ameonyesha kupagawishwa na hilo na kumtaka Mchezaji huyo atoe uamuzi wake wa kuhamia Chelsea ndani ya Masaa 48.
Monday, August 26, 2013
KAZE NA TAMBWE KUTAMBULISHWA RASMI JUMAPILI WIKI HII KWA MASHABIKI WA SIMBA
Warundi, beki Kaze Gilbert na
mshambuliaji Tambwe Amisi watawekwa hadharani mbele ya mashabiki wa timu ya Simba mjini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii katika mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya Mafunzo
ya Zanzibar, utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam
George Wakuganda, ambaye ni mwandaaji amesema mchezo huo ni maalum kwa wapenzi wa Simba SC wa Dar es Salaam kuwashuhudia nyota hao wakiichezea timu yao kwa mara ya kwanza baada ya kukamilisha taratibu za ITC.
George Wakuganda, ambaye ni mwandaaji amesema mchezo huo ni maalum kwa wapenzi wa Simba SC wa Dar es Salaam kuwashuhudia nyota hao wakiichezea timu yao kwa mara ya kwanza baada ya kukamilisha taratibu za ITC.
Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj
Ismail Aden Rage alikwenda Burundi kufuata ITC za wachezaji hao
mwishoni mwa wiki baada ya kuona zinachelewa kufika nchini.
Subscribe to:
Posts (Atom)