Tuesday, November 6, 2012

KATIBU WA MUFTI ZANZIBAR, SHEIKH FADHIL SORAGA AMWAGIWA TINDIKALI


Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba cha Huduma ya Kwanza katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
 Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye Gari la Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya taifa Muhimbili Dar es Salaam baada ya kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Wananchi mbalimbali wakishuhudia Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga akiwahishwa katika Hospitali ya taifa Muhimbili Dar es Salaam baada ya kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
(Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar)

STORI YA NYANGUMI ALIEJERUHI WATU


Nyangumi.
Watu watatu wamejeruhiwa huku mmoja wao ndio akiwa kajeruhiwa sana baada ya Nyangumi kuibuka ghafla na kurukia boti waliyokua wakisafiria huko Eastern Cape Afrika Kusini.
Boti ilikua inakwenda polepole ghafla Nyangumi akajitokeza toka chini ya maji na kurukia hiyo boti, waliojeruhiwa ambao baadae kidogo waliokolewa na kikosi cha uokoaji ni mzee wa miaka 41 na abiria wengine wenye umri wa miaka 25 na mwingine 35.




HOJA YA UHABA WA MAFUTA YAWAKIMBIZA WAZIRI MUHOGO NA NAIBU WAKE BUNGENI LEO.


Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika bungeni leo akiwasilisha hoja kuhusiana na Uhaba wa Mafuta nchini.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (aliyesimama) akijibu hoja ya Mh. John Mnyika.
Na. Mwandishi wetu, Dodoma.
Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akihoji kiti cha spika juu ya serikali kushindwa kuleta bungeni kauli ya serikali juu ya mkakati wa serikali kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini Tanzania.
Uhaba wa mafuta leo umewakimbiza kwenye kikao cha bunge mjini Dodoma asubuhi, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na naibu mawaziri wake George Simbachawene na Steven Masele.
Waziri huyo na naibu mawaziri wake hawakuwepo bungeni leo wakati Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika alitaka serikali itoe sababu ya kutokuja bungeni leo kutoa tamko la serikali ya jinsi inavyoshughulikia swala la uhaba wa mafuta nchini.
Spika wa Bunge Anne Makinda alimlazimisha Waziri kuu Mizengo Pinda kusimama na kujibu hoja ya Mnyika aliyemtaka Spika kulazimisha serikali ijibu hoja  yake pamoja na mkakati wa serikali wa kutatua uhaba wa mafuta nchini.
Waziri Mkuu  Mizengo Pinda alilazimika kunyanyuka nakusema kwa ufupi kuwa serikali ilikuwa ikijiandaa na kuja na hoja nzito ya kueleza umma mikakati kabambe ya kutatua uhaba wa mafuta nchini.

Vitu vinavyoweza kumfanya mwanamke aachwe na mwanaume


1. KUWA MWIGIZAJI
Uigizaji unaozungumzwa hapa siyo wa filamu lakini ni ile hali ya kujitengenezea tabia ambazo siyo rasmi.
Kwa mfano wewe ni masikini lakini unajifanya ni mtoto wa tajiri au wakati mwingine unaazima nguo za watu kwa lengo la kujiweka juu na tabia za kufanana na hizo. Ukiwa mwanamke uliyependwa, usithubutu kudanganya uhalisia wako kwa kitu chochote. Wanaume hawapendi kabisa tabia hiyo.
2. KUWA TEGEMEZI
Katika ulimwengu huu tunaoishi sasa, wanaume wengi hawapendi wanawake tegemezi. Katika hili uchunguzi umeonesha kuwa wanawake wenye kazi ni rahisi kuolewa kuliko wasiokuwa na kazi. Hii ina maana kwamba wanaume hawapendi kutegemewa kwa kila kitu na inapotekea hali hiyo ni rahisi kwao kubwaga manyanga na kutafuta penye unafuu. Kamwe usikubali kuwa mwanamke wa "nitumie Vocha" naomba hiki "naomba kile" kila siku utaachwa.
3. USIKIVU
Ingawa tafiti zinaonesha kuwa wanawake huzungumza zaidi kuliko wanaume, ukweli unabaki kuwa wanaume hutaka kusikilizwa katika machache wanayosema au kuagiza. Endapo mwanaume atakuwa akisema jambo fulani na mwanamke haoneshi usikivu,ni rahisi kwake kufikiria kuwa anadharauliwa na hivyo kuamua kuachana na mwanamke huyo. Kwa mantiki hiyo, wanawake wanatakiwa kuwa wasikivu kwa wanaume vinginevyo watajiweka katika mazingira ya kuachwa
4. MATUMIZI MAKUBWA
Inawezekana jambo hili linasababishwa na ugumu wa maisha ambao umewafanya wanaume wengi kubana matumizi. Inapotokea mwanamke akawa na matumizi makubwa ya fedha na vitu.,humkera mumewe/mpenzi wake. Ewe dada/mwanamke, katika kulinda uhusiano wako jitahidi kuhakikisha kuwa matumizi yako yanakuwa ya chini kuanzia mnapotoka 'OUT' na mumeo mpaka kwenye fedha za matumizi ya nyumbani unazoachiwa.
5. UBINAFSI
Maisha ya mapenzi yanataka umoja. Wanaume wanaamini sana kwenye hili hivyo wanapoona wenza wao wamekuwa wabinafsi katika mafanikio au mipango yao ya kimaisha, huingiwa na wasiwasi na kuhisi kuwa hawapendwi. Ikifikia hatua hii, huamua kujitoa kama njia ya kujihami au kutetea uanaume wao.
6. KUMTAFSIRI
Wanawake wengi wamekuwa na tabia ya kuwatafsiri wanaume kadiri wajuavyo wao bila umakini: "NILIJUA ULIPOSEMA HIVYO ULITAKA NIONDOKE". Wanaume huamini kuwa wao ni walimu hivyo linapotokea suala la mwanamke kushindwa kuelewa na kutafsiri maneno kinyume na lengo la mhusika, hujiweka kwenye kundi baya la uelewa mdogo na hivyo kujiongezea hatari ya kuachwa. Unapokuwa kwenye mazungumzo na mumeo, usimtafsiri na endapo hilo litatokea basi jitahidi kutafsiri kwa usahihi kile alichokiongea
7. KULAZIMISHA VITU
Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume hawapendi kulazimishwa kufanya mambo na inapotokea mwanamke akaweka msukumo mkubwa wa kuhakikisha mwanaume anatekeleza kitu fula(bila kujali umuhimu wa jambo lenyewe) ulazima huo hugeuka kuwa kero inayoweza kumfanya apoteze penzi lake. Ushauri kwa wanawake ni kwamba hata kama jambo fulani lina umuhimu, wasiweke lazima yenye kukera.
8. KUTENDA KINYUME
Mfano..MUME anakupatia sh. 10,000 kwa ajili ya kuchukua unga kwa ajili ya matumizi ya baadae..lakini inatokea kwamba mume anaporudi na kuulizia anaambiwa hoo! Walikuja wageni nikaamua kununua kuku na kupika...kwahiyo tabia inaweza kumfanya mume aone kuwa unaenda kinyume na ki2 alichokipanga!.. Kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kumpigia mume wako simu na kumuuliza na kumwambia kuwa kuna wageni, na umwombe kui2mia pesa ile, akikataa pika chakula chochote kile tofauti na kwenda kununua vi2 vya gharama uonekane/muonekane mnakula vizuri..hiki ki2 kinawakera sana wanaume.

KUTOKANA NA ONGEZEKO LA BEI ZA MAFUTA JIJINI MBEYA, VIJANA WAFUNGA BARABARA KUU IENDAYO ZAMBIA ENEO LA MAMA JOHN KWA MUDA WA SAA MOJA KABLA YA WANAUSALAMA KUWASILI.. SHUHUDIA

























MAISHA KIBURUDANI ZAIDI....
Kourtney Kardashian And Scott Disick Pack On The PDA

Kourtney Kardashian And Scott Disick Pack On The PDA

Kourtney Kardashian and Scott DisickKourtney Kardashian and Scott Disick

Kourtney Kardashian and Scott Disick
Kourtney Kardashian And Scott Disick Pack On The PDA 
Kourtney Kardashian And Scott Disick Pack On The PDA

No comments:

Post a Comment