Mkurugenzi msaidizi maendeleo ya michezo, Juliana Matagi Yassoda akibadilishana mawazo na mwandaaji wa mashindano Diwani Zacharia Isaya Mabwai, wakati mchezo wa fainali ukiendelea na mwali akiwa mezani kama unavyoshuhudia..
Station Manager wa redio Nyemo fm 97.7, Hezron Mwandambo akifurahi baada kutunikiwa cheti cha shukrani kwa mchango wa kutangaza mashindano hayo, mara tu baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi..
Mkurugenzi msaidizi maendeleo ya michezo-Yassoda, akisaini kitabu cha wageni kabla ya fainali kuanza
Kushoto ni mwenyekiti wa mashindano ya Mabwai supercup,katikati ni mdau wa mashindano hayo Mhadhili msaidizi Uchumi na sera katika chuo cha mipango (IRDP)-Dodoma, na kulia ndiye mwandaaji wa mashindano ya MABWAI SUPER CUP 2013 Diwani wa kata ya Sanza iliyopo wilayani Manyoni mkoa wa Singida Mh. Zacharia Isaya Mabwai
TAYARI KWA MCHEZO.Wenye jezi nyekundu zilizokolezwa na rangi nyeupe na kaptula nyekundu ndiyo walikuwa mabingwa watetezi Kijiweni fc ambao jana walishindwa kutatamba katika fainali hizo baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Sanza fc wenye waliotinga jezi zenye mchanganyiko wa rangi blue na Nyekundu.. kulia
MICHUANO hiyo ya mabwai super cup ambayo hufanyika kila mwaka kwa takribani miaka tisa sasa fainali zake zimechezwa jana katika uwanja wa Shule ya msingi Sanza katika kata ya Sanza wilayani Manyoni mbele ya mgeni rasmi Mkurugenzi msaidizi maendeleo ya michezo,Juliana Matagi Yassoda kwa niaba ya naibu waziri Habari, vijana,utamaduni na michezo Amosi Makalla, ambaye alipata dhalula na kushindwa kuhudhulia fainali hizo hapo jana.
Kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali hizo mgeni rasmi kutoka idara ya habari, vijana, utamaduni na michezo Juliana Yassoda aliwaasa vijana na wachezaji kwa ujumla kati ya timu zote zilizoshiki na ambazo hazikushiriki michuano ya Mabwai Cup, kuwa na moyo wa kujitoa na kuipenda michezo hasa mpira wa miguu kwani licha yakuwa ni burudani,Lakini pia ni ajira na husaidia kuleta mahusino mazuri kati ya vijana, wazee,watoto na vingozi mbalimbali wa vyama na serikari.
Yossada, alisema kwa upande wa vingozi wa timu na waandaaji wa mashindano wakiwemo wachezaji na waamuzi kuzingati sheria za mpira wa miguu kama zinavyosomeka na kutambulika na vya vya soka nchini na hata Duniani.
Mara baada ya salaam hizo mtanange wa fainali kati ya Kijiweni fc na Sanza fc ulinza rasmi chini ya waamzi kutoka wilaya ya Manyoni ambao wanatambulika na chama cha mpira wilaya ya Manyoni(MADIFA), Richard Robert mwamuzi wa kati akisaidiana na wenzake line one, Peter John na Ally Mohamed.
Katika fainali hiyo timu ya Sanza walionekana kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa huku wakipoteza nafasi nyingi za magoli, ambapo kwa takribani dk. 45 za kwanza walikuwa wakiliandama lango la Kijiweni fc bila ya kupata goli hii ikiwa ni kutokana na kazi nzuri ya golikipa wa kijiweni fc akitumia uwezo binafsi. Jitihada za kila timu kupata walau goli kwa kipindi cha kwanza ziligonga mwamba na kujikuta wakimaliza 45 za kwanza bila timu yoyote kuchungulia lango la mpinzani wake.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu huku timu ya kijiweni ikionyesha makucha makali tofauti na kipindi cha kwanza bidii ambazo zilizaa matunda mnamo dakika ya 55 kijiweni ikapata goli kupitia kwa Ayub Saula, Dk. 15 baadae Sanza wakapata goli la kusawazisha lililofungwa na Sajiloo Bonifasi.
Hakika kutangulia si kufika mara tu baada ya Sanza kusawazisha goli hilo walicharuka na kuwatesa kijiweni kwa vyenga na kuonyesha uwezo wao katika kusakata kabumbu, Dk. ya 85 kasoro dk tano tu ili kumalizika kwa mchezo Joseph Mwaluko akawanyanyua mashabiki na wapenzi wa timu ya Sanza kwa kuiandikia timu yake goli la pili ambalo lilidumu hadi kipenga cha mwisho na kuwafanya Sanza fc kuwa mabingwa wa Mabwai cup 2013.
Timu zilizoshiriki ligi hiyo ni Sanza fc, Kijiweni fc, Ntope,Chichecheho,Cobla,Pepeani fc na Makuru rangers, ambapo mshindi Sanza fc alipata kombe,jezi seti moja na sh.150,000/= Mshindi wa pili mpira mmoja na shs.100,000/= wakati mshindi wa tatu akilamba kifuta jasho cha sh.50,000/=
Pamoja na zawadi hizo pia kulikuwa na zawadi za vyeti kwa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kujitokeza kusapoti ligi hiyo kwa namna yoyote ile.
No comments:
Post a Comment