Diwani
wa Kata ya Dodoma mjini, David Madole akimkabidhi Kikombe nahodha wa
timu ya Atlantic mara baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya
Safari Pool ngazi ya mkoa, Mkoa wa Dodoma yaliyo malizika mjini hapo
mwishoni mwa wiki.
***** *****
TIMU
ya mchezo wa pool ya Atlantic yenye makazi yake Majengo Mjini
Dodoma, ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya pool ya 'Safari
Lager National Pool Championships 2012' baada ya kuibamiza klabu ya
Florida yenye makazi yake Barabara ya Bahi, 13-8 katika mchezo wa
fainali wa mashindano hayo ngazi ya mkoa yaliyofanyika katika Klabu ya
Atlantic mjini Dodoma
Atlantic ilitwaa ubingwa huo na kujinyakulia fedha taslimu Sh.700,000 na Kikombea mbapo pia kuwa wawakilishi wa mkoa huo katika fainali za Kitaifa zitakazofanyika Septemba 26 mwaka huu mkoani Mwanza kwa kushirikisha vilabu 16 ambavyo vitakuwa mabingwa kwenye mikoa yao.
Florida
ilikamata nafasi ya pili na kuzawa kitita cha shilingi 350,000 na
mshindi wa tatu katika mashindano hayo ni Klabu ya Tiger yenye makazi
yake eria C, ambao walizawadiwa shilingi 200,000 na wanne ni klabu
ya Car Wash ya Bara bara ya Bahi ambao walizawadiwa shilingi 100,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanaume), Abdu Forty kutoka klabu ya Florida alitwaa ubingwa kwa kumchapa Athuman Gora wa klabu ya White Horse 4-0, na kujinyakulia kitita cha shilingi 350,000 ambapo Abdu Forty alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 200,000, wakati Mohamed Jafari wa Klabu ya Atlantic alikamata nafasi ya tatu na kuzawadiwa shilingi 150,000.
Upande
wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanawake),Monica Simule alitwaa
Ubingwa na kuzawadiwa Shilingi 250,000/= na nafasi ya pili ni Happy
Mkumbo.
Zawadi kwa washindi wote zilikabidhiwa na Diwani wa Dodoma Mjini, David Madole ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo katika Mkoa Dodoma.
KISURA WA DODOMA NA POZI TATA...........
No comments:
Post a Comment