Wanahabari wakiandamana kuelekea Viwanja vya Jangwani leo asubuhi kulaani mauaji ya mwanahabari mwenzao, Daudi Mwangosi..
WANAHABARI jijini Dar es Salaam leo wameandamana kutoka Kituo Cha
Televisheni cha Channel Ten na kuhitimisha maaandamano yao katika
Viwanja vya Jangwani kwa ajili ya kulaani mauji ya kikatili aliyofanyiwa
mwandishi mwenzao, Daudi Mwangosi wa Kituo cha Chanel Ten mkoni Iringa.
Katika Maandamo hayo Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emannuel Nchimbi
alifika Viwanja vya Jangwani kupokea maandano hayo lakini alitimuliwa na
wanahabari.
WAZIRI NCHIMBI AZOMEWA AFUKUZWA KATIKA MAANDAMANO YA WANAHABARI JIJINI DAR ES SALAAM
Katika ya
hali isiyo ya kawaida wanahabari jijini Dar es Salaam wamemzomea na kumfukuza katika
maandamano ya Kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi Leo jijini DAR.
Hatua
hiyo imetokea baaada ya waziri huyo wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kufika
katika viwanja vya jangwani kwa ajili ya kujipa jukumu la kupokea maandamano
bila mwaliko.
Kutokana na zomea zomea hiyo ya wanahabari hao dhidi ya
waziri NCHIMBI hali ilionekana kuwa si shwari na kupelekea waziri huyo
kuondolewa na Rais wa UTPC Keneth Simbaya na viongozi wengine wakiwemo askari
polisi.
Wakati hayo yakiendelea huko mkoani Mara jeshi la polisi lateka
ofisi ya waandishi wa habari Kama njia ya kushinikiza wasifanye maandamano yao.
Mr. Meena akigojiwa na wanahabari wenzake
MAANDALIZI YA FIESTA 2012 MKOANI DODOMA YAANZA.
No comments:
Post a Comment